Posts

Showing posts from February, 2010

Shikamoo tumeienzi, isiwe viboko jamani!

Image
Lundo la fimbo kwa ajili ya kuwachapia wanafunzi.


Hapa ni ofisi ya waalimu ktk shule moja ya sekondari ktk wilaya ya Hai, na mlionalo ni lundo la fimbo kwa ajili ya kuwaadabisha wanafunzi. Binafsi nilipoliona rundo hilo nilistaajabu kwa kweli. Nilipata taswira ya jinsi mababu zetu walivyokuwa wakichapwa kwa makosa ambayo hata hayakustahili bali wakoloni walifanya hivyo kwa minajili ya kunyanyasa tu na kuwafanisha mababu zetu na wanyama. Binafsi naamini kuwa wanafunzi wanaweza kuelekezwa yale yafaayo na wakaelewa bila ya viboko! Adhabu mbadala ambazo zitawajenga kiakili na kimaisha hazina budi kutumiwa kuliko kuendelea kuenzi unyanyasaji huu ambao wakoloni waliutumia kuwashurutisha na kuwatesa waafrika.

Wewe ungekutana na hali hii katika ofisi mojawapo ya shule ya sekondari ungelifanya nini?