Posts

Showing posts from September, 2009

Kutoka Bloguni.

Ni dhahiri kuwa mengi yaandikwayo na kuzungumzwa kwenye blogs zetu hayawafikii watu wengi ipasavyo.Wengi wanaosoma yanayoandikwa bloguni ni wale wenye internet access katika kompyuta na wenye uwezo wa kuzitumia pia.Wimbi la hali ngumu ya maisha lasabisha wachache kuweza kwenda kwenye internet cafe ili kuweza kutumia intenet.Mbali na niliyoyaeleza hapo juu, ufahamu wa blogs ni mdogo kwa jamii kubwa ya watu.

Ili kuhakikisha kuwa asilimia kubwa ya watu wanazifahamu blogs na angalao kuweza kupitia yaliyoandikwa(hata kama ni blogs chache) kuna jambo moja ambalo nalifikiria.Yawezekana hili lilishadokezwa lakini si vibaya nikilikumbushia.


Wazo hili ni la kubandika post fulani kwenye magazeti kutoka katika blog yoyote ilimradi tu post ile iwe ni ya kufunza au kuburudisha jamii.Si tu kwenye magazeti,hili lawezekana hata kwenye vituo vya televisheni na vituo vya redio,kwani naamini sehemu hizi zina huduma za internet.Kwa hiyo blog inaweza kufunguliwa na ikasomwa na hatimaye yaliyoandikwa kuwafiki…