Posts

Showing posts from August, 2009

Kuelekea uchaguzi mkuu.

Waonaje kama wananchi kwa pamoja wakikusanyika pamoja ili kujadili na kuchambua sera moja baada ya nyingine za wagombea watakaopita katika eneo lao ili kutambua kama sera hizo ni hai,zatekelezeka na zitawafaa na kuwafikisha mbali kimaendeleo kuliko kazi hii kufanywa na mtu mmoja mmoja?


Si tu kujadili sera bali hata kuwajadili viongozi wenyewe juu ya utendaji wao wa kazi,ufanisi,kama walishakuwa viongozi, walifanya nini na mambo kama hayo ambayo yataweza kutusaidia katika kuwapata viongozi bora na ambao ni wazalendo.


Naomba niliwasilishe hili kwenu na tulijadili kwa pamoja.

Wito kwa wazazi/ walezi.

Inafahamika kuwa waislam wote wako katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.Mfungo huu huwahusisha watu wazima na watoto.Kwa upande wa watoto wale wanaosoma nimegundua kuna tatizo.Wanafunzi wanalala madarasani na wakiulizwa wanasema wamefunga.Wengine hulalamika kwa maumivu ya tumbo na hivyo kushindwa kuzingatia masomo ipasavyo.
Kimsingi wale wote wanaofunga wanatakiwa wawe na furaha wakati wote na taratibu za kawaida za kila siku hazitakiwi kukwama kwa kigezo cha kufunga.
Hivyo wazazi wawe makini na watoto wao,wawaelekeze yapi ya kuzingatia kwa wale wanaofunga.Pia wazazi lazima wawe makini kwani kuna watoto wasioweza kuhimili mfungo hivyo wazazi hawana budi kuwatambua na kuwaelekeza nini cha kufanya.Nawatakia waislam wote mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

"Sidanganyikii!!"

Sio mimi nasema hivi bali ni kijana wa kike ambaye huwa anasikika kwenye vituo mbalimbali vya redio na pia kuonekana kwenye vituo vya televisheni.
Kijana huyu anasikika na kuonekana katika tangazo ambalo limethaminiwa/andaliwa na Umoja wa wanahabari wanawake Tanzania.Tangazo hili linawafundisha watoto wa kike hususani wa shule za msingi kukataa ofa zitolewazo na wanaume ambao lengo lao ni kuwahadaa KIMAPENZI.
Binafsi huwa napata maswali mengi kutoka ktk tangazo hili.
Huwa najiuliza kama neno "sidanganyiki" ni rahisi kutoka kwa mtoto wa kike ambaye hana malezi bora.Mbali na hilo kuna changamoto za umasikini zinazomkabili kijana huyu kama za kifedha, lishe bora,n.k. Sasa kwa hali hii "sidanganyiki" itaweza kutoka kweli na atamkaye atakuwa anamaanisha kweli? Kuna wakati miili yao inawatuma na kwa upande mwingine wako wanaume wakware na vijizawadi vidogovidogo.Kwa hali hii kijana huyu hawezi kushawishika na kuona kuwa ni neema juu yake kwani mbali na kutaka kutimiza mata…

Hofu ipo kwa watoto

Katika blog yangu ya Mashairi(mashairi-kissima.blogspot.com) niliandika shairi lililokuwa na kichwa cha habari kinachosema "dini zetu ni kikwazo".Nilieleza jinsi dini inavyoweza kuwa kikwazo kwa wapendanao,pia wazazi wasivyokubaliana na watu wa dini tofauti kuoana.
Nawashukuru wale waliochangia.


Nadhani si tatizo sana kwa wawili wale wa dini tofauti kuishi pamoja bali changamoto kubwa inakuja kwa watoto watakaozaliwa.Msimamo wao kiimani utakuwa ni upi kama wazazi watakuwa na dini tofauti?.Ni dhahiri kabisa kuwa wapo wenye uzoefu na hili au wapo waliokwisha kuishi au kuwa karibu na familia za mchanganyiko huu.Mchango wenu wa kimawazo ni wa muhimu sana kwani utasaidia sana si tu kuweka imani kubwa kwa msemo huu "mapenzi hayachagui dini" bali pia kunusuru mahusiano ya wapenzi walio ktk imani tofauti za kidini.Karibuni tuweze kulijadili hili kwa kina.