Posts

Showing posts from June, 2009

Kisa mkasa

Hodi tena ndani humu,
salamu ndugu salamu,
hakika kitu muhimu,
kisha tegeni yenu,
masikio jama kuna kitu,
kipi kilonisibu,
kipi kisa na mkasa.


Siku zilipita,
bloguni sikupita,
katu sikujificha,
mtandao sio kisa,
majukumu kisa mkasa.Aliuliza dada Yasinta,
moyoni wengi walijiuliza,
kulikoni Kissima,
bloguni kakosekana,
namba moja fungu latanabaisha,
majukumu kisa mkasa.


Kwa kishindo nimerudi,
mengi nitayafaidi,
hakika ya bloguni,
yatakuwa hayanipiti,
kweli tupu sijitetei,
majukumu kisa mkasa.