Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija
Picha: Blogger. Upimaji endelevu wa mwanafunzi ndio namna pekee ya kutoa taarifa za maendeleo ya ujifunzaji wa mwanafunzi katika kufikia malengo ya ujifunzaji yaliyokusudiwa kwake. Kwa hiyo, upimaji endelevu ni shuhguli ya msingi mno ya kuzingatiwa na mwalimu na wanafunzi. Upimaji endelevu siyo shughuli ya mwalimu peke yake. Ni mchakato wa pamoja kati ya mwalimu na manafunzi. Hii ni kusema kuwa, upimaji endelevu ni sehemu ya ujifunzaji wa mwanafunzi na ufundishaji wa mwalimu. Ikiwa tunahitaji kuona upimaji wenye tija, basi kila mmoja ni lazima atimize wajibu wake kwa kushirikiana. NWEA katika chapisho lao la mwaka 2016 linaloelezea mambo makuu manne ya kuzingatia ili kuleta ufanisi kwenye upimaji endelevu, wanaeleza kuwa upimaji endelevu ni mchakato wa pamoja kati ya mwalimu na wanafunzi wa kukusanya ushahidi wa ujifunzaji wa wanafunzi kwa lengo la kuboresha kile kinachoendelea darasani, kwa maana ya mchakato wa ujifunzaji wa wanafunzi. Ili...