Posts

Showing posts from March, 2011

Inatosha sasa kuona, bora mimi kusema: Serikali yangu iharibuyo kioo itegemeacho kujitazamia.

Image
Ni siku nyingine ya Jumamosi ambapo blogu yako ya Mwangaza inakuletea kipengele cha "Inatosha sasa kuona, bora mimi kusema".

Naam, wiki hii tarehe nane mwezi huu, wanawake duniani waliadhimisha siku yao almaarufu Siku ya Wanawake duniani. Hapa Tanzania, kilele cha maadhimisho hayo yalifanyika pia, kama ilivyozungumziwa hapa katika tovuti ya Startv.
Sina hakika sana kama maadhimisho haya yalifanyika kuanzia ngazi ya kijiji hadi kitaifa. Mimi katika pitapita yangu ya kimajukumu, nilikumbana na maadhimisho hayo katika shule ya msingi Tumuli iliyopo wilayani iramba mkoani Singida, pamoja na kuwa sikuwa na muda mwingi wa kufuatilia maadhimisho hayo.

Mgeni rasmi alikuwa mkuu wa Wilaya ya Iramba akiwa na msafara wake uliosheheni vigogo mbali mbali wa chini yake.
Mengi yaliongewa na kukamilishwa na kauli mbiu isemayo "Fursa sawa katika elimu,Mafunzo na Teknoloji:Njia ya wanawake kupata ajira bora" ambayo ndiyo kauli mbiu ya siku ya wanawake kwa mwaka huu. Iinigusa sana …

Inatosha sasa kuona, bora kusema (Serikali ya Tanzania na usaliti kwa walipa kodi wake)

Image
Kadiri siku zinavyoenda, nazidi kujionea namna ambavyo serikali yangu ya Tanzania inavyoonesha udhaifu mkubwa katika masuala mengi ya utendaji wake. Katika pita pita zangu, nilikutana na jengo moja lililopo katika kijiji cha Kyalosangi kilichopo wilaya ya Iramba katika tarafa ya Kinampanda mkoani Singida. Nililisogelea karibu na kisha nilikiona kibao kama kinavyoonekana hapa chini  katika picha ambacho kilinitambulisha kuwa ni mahakama ya mwanzo. Nilistaajabu maana jengo hili linaonenaka kama ni gofu na ni mda mrefu sana umepita bila kutumika. Nilfanikiwa kuomgea na mkazi mmoja na alinieleza kuwa mahakama hii inatumika na kwa bahati nzuri nami siku moja nilishuhudia watu wakipata huduma mbalimbali katika mahakama hii iliyo katika hali ya kusikitisha kwa namna jengo hili lilivyochakaa kana kwamba haina uangalizi wa aina yoyote wa wananchi na serikali .


Hiki ni kibao kinachoelekeza mahali ilipo Mahakama ya Mwanzo, Kinampanda wilayani Iramba katika Mkoa wa Singida.

 Picha hapa juu ni mwone…

Inatosha sasa kuona, bora kusema-Kipengele kipya

Mwanamuzki wa kizazi kipya ndugu Joseph Haule anayejulikana sana kwa jina la Prof J aliwahi kuimba wimbo uitwao INATOSHA SASA aliomshirikisha mwanamuziki wa siku nyingi Joseph Mbilinyi almaarufu kama Mr Sugu ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Mbeya Mjini. Prof J kuna sehemu anasema "inatosha sasa kuona nadhani bora mimi kusema" Prof J anaonesha kukerwa na mambo ambayo hayampendezi yeye, na pia yasiyoipendeza jamii vilevile. Mwanafasihi huyu anatukumbusha kuwa ifike mahali sasa tusiishie tu kuona uovu, bali na tuusemee kwa usahihi wake kwani pia ni hatua nzuri katika kutatua au kuuondoa uovu huo. Dhana hii pia si vibaya ikitumika hata kwenye mazuri katika jamii katika harakati za kuwapa moyo wale wote wenye kutenda kwa kadiri ya inavyotakiwa.


Umefika sasa wakati hata wanajamii wote, mmojammoja na hata kwa umoja wetu, tusiishie kuona tu, umefika muda wa kusema wazi kuwa haturiridhiki na huduma, haturidhiki na utendaji. Pia hatuna budi kusema pale tunaporidhika; lakini kikubwa hapa ni…