Posts

Showing posts from December, 2009

Kikao cha dharura

"Mawasiliano", kitaalam wanaita "communication"

"utunzaji wa mazingira" kitaalam wanaita "environmental conservation"

"kiziwi" kwa lugha ya kitaalam wanaita "deaf"

"Kichocho" kwa lugha ya kitaalam wanaita "Bilhazia"

"kukohoa" au kwa lugha ya kitaalam "coughing".
"mmen'genyo wa chakula" au kitaalam "food digestion"

Mifano ni mingi, na watu wengi huwa wanafanya hivi mara kwa mara. Najiuliza ni kwa nini lugha ya kitaalam iwe ni Kiingereza. Binafsi sipati mantiki ya tafsiri hii ya kubadilisha maneno kiswahili, pengine yaliyojitosheleza na kuyapeleka kwenye lugha nyingine( kiingezera) na kisha kulitunuku neno hilo kuwa ni la kitaalam. Likiwa katika lugha ya kiswahili , haliitwi la kitaalam.

Sijui niite ni dharau za wazi kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili, au ni ishara ya wazi ya upungufu wa uzalendo tulio nao?
Binafsi bado sijapata maana halisi ya kwa nini maneno ya kiswahi…

Tanzania; tuwezeshwe kujitafutia fedha na si kupewa fedha!

Tanzania ni kati ya nchi nyingi barani Afrika ambazo hutegemea sana ufadhili wa kifedha kutoka nchi za Magharibi. Asilimia nzuri tu ya bajeti ya Tanzania inatoka na ufadhili huu. Misaada mingi ya kifedha kwa bahati mbaya imekuwa ikielekezwa kwa mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yamekuwa si ya kutuwezesha kupiga hatua ya kimaendeleo bali kujaribu kutusaidia mizigo mbali mbali. Misaada mingi imekuwa ikielekezwa kwenye vita dhidi ya ukimwi na Malaria. Pamoja na jitihada hizo bado idadi kubwa ya watu wanaangamia kwa magonjwa haya na mengine.

Ninachojiuliza hapa ni kwamba ni kwa nini wasitujengee misingi ya kuweza kujitegemea kuliko kutupa fedha na kisha kutupumbaza kuwa sisi ni masikini tunaohitaji kusaidiwa kila saa na dakika?

Kwa nini wasitujengee viwanda vya kusafisha na hatua nyingine sipasayo madini kabla ya kuingia sokoni?

Kwa nini wasituboreshee viwanda vyetu ili tutumie malighafi lukuki tulizo nazo hapa nchini?
Kwa nini wasiboreshe njia za mawasiliano kama mabarabara ili maen…