Posts

Showing posts from November, 2009

Peruzi blogs kiganjani mwako!

Dunia sasa imekuwa kama kijiji, au niseme kamtaa fulani hivi.Ikidhaniwa kama ni mduara basi naweza kusema kuwa kipenyo chake kimepunguzwa kwa kiwango kikubwa kabisa. Twashukuru, ukuaji wa teknolojia ya intaneti umefanikisha hili kwa kiasi kikubwa kabisa.

Mwanzoni, miaka kadhaa iliyopita teknologia ya intaneti ilikuwa ni kwenye kompyuta tu, lakini hivi sasa huduma hii ipo hadi kwenye simu za viganjani.Uwezo wake wa kufanya kazi unategemea na uwezo wa simu yenyewe. Unaweza kutuma email,kupokea jumbe za email, online chat,unaweza kufungua tovuti yoyote na ukasoma vilivyomo na mambo mengine mengi yahusuyo intaneti. Kwa mantiki hii hakuna atakayeshangaa nikisema inawezekana kutembea huku ukiblog, yawezekana kupitia blogs za wadau mbalimbali kupitia mtandao wa simu. Waweza kuweka posti, hata kuanzisha blogs kupitia mtandao huu wa simu. Inawezekana. Unaweza kuongeza ufanisi wa simu kwa kutumia phone applications ambazo zinaonekana ni msaada mkubwa hasa kwa upande wa blogs. Najua wapo wan…

Ukosefu wa UZALENDO, sumu ya Mafanikio Tanzania.

Tanzania ni nchi ambayo imebarikiwa kwa kuwa na rasilimali za kutosha kabisa ambazo zikitumika vizuri zinaweza kubadilisha hali mbaya ya uchumi na umasikini tulionao watanzania tulio wengi.

Hali ya "umimi" kwa viongozi wengi wa serikali inakithiri kila kukicha, hili lajidhihirisha kwa namna watu wanavyotumia kila mbinu kupata uongozi kuliko kutafakari hali halisi ya watanzania.Watu wanazitafuta nafasi za uongozi kwa manufaa yao binafsi na kulisahau taifa. Tujiulize viongozi wastaafu mathalani maraisi,wana mchango gani baada wao kuachia ngazi? Wengine wanasahaulika kabisa kama walishakuwa maraisi!Hivi baada ya Nyerere kung'atuka alipotelea mitini kabisa? Umimi, ukosefu wa "uzalendo" kwa viongozi wetu ni tatizo kubwa na ni sumu ya maendeleo.

Wananchi nasi twahitaji kuwa wazalendo pia.Yashangaza sana,tena sana kwa baadhi ya wananchi kushabikia chama kuliko uwezo wa mgombea ktk uongozi. Utamsikia mtu anasema mimi ni CCM damdam kwani kila mwaka inashinda tu,hawashi…