Posts

Showing posts from October, 2009

Nimechoka!

Sijachoka kuelimisha, sijachoka kuelimishwa,sijachoka kuburudisha!


Lakini!


Nimechoka na ubabaishaji wa huduma za serikali.BiMA YA AFYA kwa mfano,utaambiwa ugonjwa huu bima ya afya haiwezi kutibu, dawa hizi,kwa bima ya afya hutaweza kuzipata, walazimika kwenda kununua! Msaada wake nini sasa! Kweli nimechoka!


Nimechoka na sera nzuri na zenye mvuto kwa kuandikwa na kusemwa tu pasipo kuwa na utekelezaji.Sitamani kuzisikia wala kuzisoma popote tena! Miaka arobaini na saba na bado hatuoni nafuu! Mimi nimechoka kwa kweli!


Nimechoka kumpa kura ya kwenda kula mbunge wangu.Huwa namwona wakati wa chaguzi tu. Nikijaribu kufikiria kwa kipindi cha miaka yote ya ubunge kanifanyia nini ambacho atakapokuja tena kuomba kura atajivunia nacho na wananchi watafurahi kumwona tena, sikipati.Binafsi nimechoka! Nimechoka!


Umeme wakosekana masaa ishirini na matano na si mara moja kwa wiki!.Hakika haya ni masihara! Kwa hali hii lazima ningechoka tu!
Na nimeshachoka.

Ni kweli chama kimoja chashinda kwa halali miaka …