BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU, Mmh!

Hivi karibuni bodi ya mikopo ya elimu ya juu imetangaza kuwapa ufadhili wa asilimia mia kwa wanafunzi wa elimu ya juu watakaojiunga kwenye vitivo vya SAYANSI.Utaratibu huu umepangwa kuanza mapema mwezi wa tisa mwaka huu kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza 2009/2010
Bila shaka mpango huu umechukuliwa katika mitizamo tofauti tofauti kulingana na interests za kila mmoja. Wapo walioufurahia bila shaka wote wale watakaojiunga na vitivo vya sayansi na pia wapo wale ambao hawajaridhika na mpango huu pengine wakiwemo wale ambao hawasomi masomo haya ya sayansi.


Kwa mujibu serikali, sababu hasa ya kutoa kipaumbele hiki ni kuwahamasisha wanafunzi wengi wajiunge na masomo ya sayansi ili hatimaye wapate wataalamu wengi ktk fani hii.Binafsi hapa ndipo hasa pamenifanya nigune.


Hivi wanafunzi hawa wanaopewa asilimia mia ya mkopo wanajua mazingira waliyopitia?

Kipaumbele kinawekwa hapa juu bila kuangalia wanasayansi hawa wanaanzia wapi.Shule nyingi za sekondari hususani za kata hazina maabara, zenye maabara vifaa vyake havifai na wala hivyo visivyofaa havitoshi.Walimu wa haya masomo hawana mazingira mazuri ya kazi zao,vitabu vya ziada na kiada vya masomo haya havitoshi.
Je mwanasayansi anayeandaliwa ktk mazingira haya ataweza kukidhi haja ya wanasayansi ambao serikali inawataka.


Serikali imefanya jambo jema kuipa kipao mbele sayansi lakini sehemu waliyoweka kipaumbele hiki nadhani haikuwa sehemu sahihi.
Ningependelea sana kama kipaumbele hiki kiwekwa kwenye msingi wa masomo haya hususani kwenye shule za sekondari kwa maana kwamba mazingira mazuri ya masomo haya yaandaliwe na nadhani wanafunzi wengi watashawishika kusoma masomo haya.


Naweza kusema kuwa wanafunzi wanaojiunga na vitivo vya sayansi wamepatikana kwa bahati kwani mazingira waliyopitia yanatisha kupita kiasi na pia wanafika vyuoni wakiwa hawana msingi mzuri wa masomo haya.


Mbali na hayo inaonekana kuwa ufadhili huu wa asilimia mia ume concentrate fedha za mkopo ktk kundi moja na hivyo kupelekea wanafunzi wa vitivo vingine pamoja na vigezo vya kuwawezesha kujiunga na vyuo lakini mkopo unaweza kuwa ni tatizo.

Comments

Bwaya said…
Kissima,

Maamuzi ya serikali ya siku hizi hayaeleweki. Usishangae kesho ukaambiwa kipaumbele ni kwa wanafunzi wanaliosoma shule za kata.

Kidumu chama cha mapinduzi...
Kissima said…
Ni kweli kaka Bwaya, ndio maana hata walimu wa diploma mwaka wa pili wamewekwa pending, wako nyumbani wameambiwa waliambiwa wasubirie bajeti ya wizara ya elimu.
Wakiita chama gani "kidumu...."
Bwaya said…
...cha mapinduzi!

Baada ya shule za kata, sasaivi imekuwa Vyuo Vikuu 'vya kata.'

Sasa wasikilize wakisomeana tarakimu kwa mbwembwe...mwanafunzi milioni mbili wako sekondari...vijana laki moja wako vyuo vikuu! Utafikiri kuna cha maana kinapatikana huko kunakosingiziwa shule!

Mie huwa sielewi. Hivi katika nchi kubwa kama hii, hatuwezi kuwa na mipango inayozidi miaka mitano? Kwa nini kila kinachofanywa kinakuwa kinalenga uchaguzi unaofuata?

Nderumo, Usiwasikie wanazungumzia asilimia mia ukadhani wana jipya. Wanajua mwakani miezi kama hii patakuwa hapatoshi!
Kissima said…
Fomesheni ya 4 moja kaka Bwaya wananchi tunatakiwa kuitambua.Miaka minne walijichimbia halafu mwaka wa tano ndio wanajidai kuwa wako karibu na wananchi.

Popular posts from this blog

Mmea wa Mlonge- "Moringa Oleivera"

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.