Posts

Showing posts from July, 2009

NI KULWA AMA NI KURWA?

Wote twafahamu kuwa watoto mapacha wana majina yao maalumu ambayo ni Kurwa(Kulwa) na Doto.

Binafsi nimezoea kutumia jina la Kurwa.Lakini nilishangaa sana siku moja mtu alinikosoa na kuniambia kuwa si Kurwa bali ni Kulwa.Hapo kulitokea mabishano wengine tukisema ni Kulwa na wengine walisema huwa wanaitwa Kulwa na si Kurwa.


Wapo waliosema kuwa Kurwa limetoholewa tu na watu wa kanda ya ziwa, jina Kulwa wao hutamka Kurwa, vile vile wapo waliosema Jina sahihi ni Kurwa na hili Kulwa ni lafudhi tu ya watu wa Pwani.

Sasa nijuzeni, kipi ni kiswahili fasaha? KURWA AMA KWULWA?

WAKOLONI WALIONDOKA LAKINI MIFUMO YA KIKOLONI LEO, JANA NA KESHO.

Ukijaribu kutafakari kwa makini utagundua kuwa asilimia kubwa ya maisha yetu yanatawaliwa sana na mifumo ya kikatili ya kikoloni iliyokuwa inatumika kuwakandamiza mababu zetu.Mababu zetu walizoea hali hizi na ikawa utaratibu wa kawaida wa maisha kiasi kwamba hata baada ya kuondoka kwa wakoloni mifumo hii iliendelea na kurithiwa vizazi na vizazi.Mifumo hii ya kikoloni hadi leo hii ipo na kwa vile imeshachukuliwa kuwa ni sehemu ya maisha inakuwa ni vigumu sana kuitambua ambapo kuibadilisha kazi kubwa yahitajika.Hebu tutazame hili kwa kuzingatia maeneo yafuatayo.


MASHULENI NA MAJUMBANI.
Mwanafunzi au mtoto akikosea, fimbo hutumika kumuadhibu ili kujenga maadili.Ukatili huu ulifanywa na wakoloni kwa watu waliokuwa wanakwenda kinyume na matakwa ya wakoloni.


CHEO:
Utashangaa sana mzee anamsalimia kijana kwa vile kijana ni bosi wa mzee.Unyenyekevu ambao mababu zetu walilazimishwa kuuonyesha kwa wakoloni bila kujali umri ndicho kinachoendelea hata leo hii.Leo hii waweza kuingia kwenye ofisi ya …

BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU, Mmh!

Hivi karibuni bodi ya mikopo ya elimu ya juu imetangaza kuwapa ufadhili wa asilimia mia kwa wanafunzi wa elimu ya juu watakaojiunga kwenye vitivo vya SAYANSI.Utaratibu huu umepangwa kuanza mapema mwezi wa tisa mwaka huu kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza 2009/2010
Bila shaka mpango huu umechukuliwa katika mitizamo tofauti tofauti kulingana na interests za kila mmoja. Wapo walioufurahia bila shaka wote wale watakaojiunga na vitivo vya sayansi na pia wapo wale ambao hawajaridhika na mpango huu pengine wakiwemo wale ambao hawasomi masomo haya ya sayansi.


Kwa mujibu serikali, sababu hasa ya kutoa kipaumbele hiki ni kuwahamasisha wanafunzi wengi wajiunge na masomo ya sayansi ili hatimaye wapate wataalamu wengi ktk fani hii.Binafsi hapa ndipo hasa pamenifanya nigune.


Hivi wanafunzi hawa wanaopewa asilimia mia ya mkopo wanajua mazingira waliyopitia?

Kipaumbele kinawekwa hapa juu bila kuangalia wanasayansi hawa wanaanzia wapi.Shule nyingi za sekondari hususani za kata hazina maabara, zenye maabar…

KWA NINI HISABATI(MATHEMATICS) HUCHUKIWA?

Kwa hapa Tanzania, mathematics linaonekana na kuchukuliwa kuwa ni somo gumu.


Kimsingi sidhani kama kuna yeyote alizaliwa akiwa anajua hesabu.
Ni kwa nini utakuta yule apendaye hesabu hapendi history? Au apendaye Chemistry hapendi kiswahili? Na wakati huo huo wako wanaopenda kiswahili na Chemistry au Mathematics na histori na wanafaulu vizuri?(hapa naongelea O- level ambapo mtu anaweza kusoma masomo haya kwa pamoja)

Naamini kuwa hakuna aliyezaliwa akiwa ni wa kuja kusoma masomo ya arts au science.Mkondo ya masomo ambayo mtu atakwenda nayo inategemea tu na mazingira atakayokutana nayo pindi atakapoanza shule na hata mazingira ya atokapo.

Hali kadhalika kwa somo la hesabu, inategea sana mwanafunzi toka aanze kujua kuna hesabu alikutana na walimu wa aina gani,yani inategemea kama mwalimu wa kwanza aliweza kumshawishi vizuri mtoto ktk hesabu. Hapa namaana kwamba huyu mwalimu aliweza kumfundisha kwa uzuri yale aliyopaswa kufundishwa.Ina maana kwamba kama hakuweza kumshawishi, na mwanafunzi hu…

Naomba nikung'ate sikio.

Msingi wa penzi ni kuridhika.Ukiridhika naye utamjali, utamlinda,hutompa sababu za kumpenda,hutompenda kwa maneno bali utampenda kwa vitendo.

Mkubali, mpende kama ulivyomkuta,usiridhike na mazuri yake, hayo yapo, yadumishe na umwongezee mazuri.

Penzi laundika na lajengeka.

Jukwaa jipya.

Ndugu wanablog kuna jukwaa jipya nimelianzisha. Haliko mbali sana na hapo ulipo.Jukwaa lenyewe hili hapa
www.mashairi-kissima.blogspot.com.(samahanini sijaweza kuweka direct link)
Wote nawakaribisha hapa kwa MWANAMALENGA tupate kuelimika, kujifunza na pia kuburudika.
Karibuni sana.

NIPENI JIBU

Wengi hutamka mara kwa mara kuwa wanawapenda wake zao, waume zao na hata wapenzi wao. Ni vema na ni haki kabisa.

Swali: Utamwelewaje(utamchukuliaje) akuorodhesheaye sababu za kukupenda wewe?
Ni sahihi kufanya hivyo?

JE, UNAO UHURU WA KUTAFAKARI Na KUIKOSOA IMANI YAKO YA DINI?

Ukweli ni kwamba kila dini ina imani yake ambayo kimsingi kila muumini anatakiwa kuifuata.Imani hii kwa dini nyingi haupaswi kuhoji kusuhu lolote lihusianalo na imani hii.

Matokeo ya kuhoji imani hizi kila mmoja anayajua.Wapo wengi waliohoji na matokeo yake wamezikimbia dini zao na kuanzisha kama si dini mpya basi madhehebu mapya.

Mimi nadhani utaratibu huu ndio uliokuwa unatumiwa na wazungu kwamba unatakiwa kukubali tu bila kuhoji lolote.

Dini zinatakiwa zibadilike kulingana na maisha yanavyokwenda.Asilimia kubwa ya watu wa sasa wameelimika na wanauwezo mkubwa wa kupambanua mambo na kujua uongo na ukweli.Dini zinatakiwa kutambua hili na kufahamu kuwa zinatakiwa kuakisi maisha halisi ya sasa na ya wakati ujao.

Kwa hali hii ya kutokupewa uhuru wa kutafakari kuhusu imani zetu ina matokeo mawili makubwa, mojawapo likiwa hili la kuanzishwa kwa dini mpya au madhehebu mapya na pia watu kuishi bila ya kufuata dini yoyote.

Je, unao uhuru wa kutafakari na kuikosoa imani yako?
Au huwa unatekeleza …

Homework ya Mwl. Klyson

Kwanza naomba mwl Klayson anisamehe kwa kutumia jina lake bila idhini na pili anisamehe kwa kuchelewa kumpa majibu ya home work aliyonipa.Home work hili alinipa kwenye mjadala uliokuwa na kichwa cha habari "JARIBU UJIONEE" ilikuwa ni kuangalia kivuli chako wakati wa mchana kwa muda na kisha kuangalia mawinguni.Basi mwalimu naye alinipa homework ya kuchora msalaba wa njano kwenye karatasi nyeupe na kisha kuungalia kwa dakika moja na kisha kufumba mcho halafu niseme nitakachokiona.Nilifanya hivyo na niona na kugundua yafuatayo.


Niliangalia msalaba huo wa nyano niliouchora kwenye karatasi ya nyeupe kwa dakika moja, ila kabla ya dakika kuisha niliona kivuli cha rangi ya Violet nyuma ya msalaba ule.Nilimaliza dakika moja na kufumba macho.Niliona ule msalaba ukiwa mdogo na ukiwa na rangi ya violet kama ya kivuli nilichokiona nyuma nya msalaba niliouchora kwenye karatasi.


Nilitumia rangi nyingine kuchora misalaba na niliona yafuatayo.
Msalaba wa rangi ya kijani niliona kivuli cha p…