Posts

Showing posts from April, 2009

Wazo la leo

"usipoteze muda wako katika kujiridhisha kuwa ninajua, bali tumia muda wako mwingi katika kuvielewa vile ninavyovijua"


Haiwezekani wewe kufanya jambo kama hili.
Mawazo haya kamwe si yako, ngoja tu, nitachunguza ili nijue kama ujuzi huu ni wako au la.

Wako watu wa aina hii, wenye kuongea ama kuwaza maneno kama haya.Watu hawa hakika hawapendi mafanikio ya wenzao wala mafanikio yao wenyewe kwani hawapendi kujifunza kutoka kwa wenzao bali wanaishia kuhakikisha kuwa fulani kweli anajua, na baadae kutafuta hata njama za kukufanya uonekane hujui.

Tafakari yangu.

"UKWELI na HADHI ya mtu, ama ya kitu, ni kama mafahali wawili wasioweza kukaa kwenye zizi moja"

Utamsikia mtu anasema "kwa vile ni wewe, la si hivyo, ungekiona cha mtemakuni, mwingine utamsikia, "ninalinda heshima yako tu, vinginevyo ningekupa ukweli"

"ningesema kila kitu ila niliamua kutunza heshima ya chama" kuna kipindi aliwahi kusema mkubwa mmoja. "hakuna haja ya kumweleza kwani atakata tamaa"

Pengine ni rahisi sana kwa uongo kutumika katika kulinda hadhi!
Tafakari kuhusu hili kwani haya ni mawazo yangu tu, unaweza kunikosoa, kuafikiana nami n.k.
Usiogope ati kisa mimi mwanablog, tunafahamiana n.k, kama hili limekugusa, changia ukifikiriacho kuhusiana na hili.

Je wajua hili?

Usishangae, ni akili ya binadamu tu, chukua kalamu, au kalkuleta, fanya hesabu hili,
chukua 259 x( umri wako) x 39 = jibu utakalopata lazima ni namba tatu zinazofanana, kila moja ikitaja umri wako bila kukosea! Jaribu kisha uniambie.,

hivii, ni kati ya siri zilizo ndani ya namba, au ni dhihirisho la uwezo wa akili ya binadamu katika kucheza na namba?

TAJIRI WA AKILI AMBAYE NI FUKARA WA KIPATO.

Umeshawahi kukutana au kuishi na mtu mwenye sifa hizi?
Watu wa aina hii wapo kweli au ni mawazo ya kusadikika?

Wewe utajivunia kuwa na sifa hizi?
Binafsi ni bora niwe na moja kati ya sifa hizi mbili.

Hili wewe unalionaje, unalizungumzia vipi?
Karibu sana.

Thamani ya Binadamu.

Binadamu ni kiumbe ambaye anastahili kupewa thamani ya hali ya juu kabisa kuliko kuliko kiumbe yeyote yule na hata kitu kingine chochote kile.


Katika dunia ya leo thamani ya binadamu imepotea kupita kiasi huku thamani hiyo ikihamishiwa kwenye vitu.Hili linajidhihirisha pale ambapo binadamu anauliwa na viungo vyake kuchukuliwa na kwenda kuuzwa ili kupata pesa.

Mbali na hilo ulimwengu wa sasa umetawaliwa na matukio mengi ya mauaji.Mfano hapa Tanzania kwenye taarifa nyingi za habari matukio mengi ya mauaji yamekuwa yakiripotiwa.Cha kusikitisha hapa ni kwamba sababu za mauaji haya ni zile za kudaiana pesa, wivu wa kimapenzi n.k., yani kuutoa uhai wa binadamu imechukuliwa ni jambo la kawaida kabisa.

Tunashuhudia pia binadamu wanavyonyanyasa binadamu wengine. Watu wanafanyishwa kazi za sulubu,mshahara mdogo na hata kutotimiziwa mahitaji muhimu ya binadamu kama chakula,malazi na hata mavazi.

Mbali na binadamu kwa binadamu kutothaminiana pia kuna binadamu wasiojithamini wenyewe.Mfano mzuri ni wal…

UKWELI NDIO HUU

Hata kama kwa sasa hutakubali,
una muda wa kutafakari,
kisha afikiana nami.


usijiite tajiri,
kama huwezi nisaidia mia mbili,
usiuweke mbele ubinafsi,
wape wenzako nafasi,
utajiri wako utaufaidi.


aliyechoka kutafuta,
labda kesha pata,
au tamaa kesha kata,
asiyeona,
labda kapofuka,
au macho kayafumba.

ukweli usipounena,
kimya lazima kitakubana,au
uongo lazima utausema,
kama nakupiga kamba,
lawama mimi nazibeba.


Thamani ya dhahabu,
zaidi ya ya binadamu,
kweli hii ni aibu,
pesa zalindwa kwa mtutu,
albino wafa kila siku,
toka lini dili likawa binadamu,
wafanyao ushenzi huu,
kwa Mungu ipo adhabu,
ukweli ndo huu.


wachache wajilimbikizia,
pesa wasizojua zilipotokea,
tena hawawezi tuhurumia,
njaa twajifia,
wao mabilioni wajichotea,
ipo siku puani yatawatokea,
tayari tumeanza jionea
na Mungu aliyejuu anatupigania.


Ulevi si wa pombe pekee,
intaneti, musiki nikwambie,
kusoma,kuandika,kula nikuhabarishe,
vyote ni ulevi utambue,
visipokuwa na kiasi nikwambie,
kote muda unalika ujue,
kote lazima pesa itumike,
hili lazima ulijue.


Uzuri wa tab…

"Hekima si umri"

Hekima uwezo binafsi,
mkubwa mdogo wote wana nafasi,
haijalishi ukata wala ukwasi,
hekima kama safari,
upana'we kama bahari,
akilini mwako tafakari,
hekima kamwe sio umri.

Maarifa'yo yeza changia,
hekima'yo kujitengenezea,
mazingira'yo kukurahisishia,
gumu kwako lajiishia,
wakubwa'ko wakutembelea,
makubwa yao kuwatatulia,
wadogo'zo wakufurahia,
mazuri'yo wayachangamkia,ukubwa zaidi heshima,
upeo waikamata hekima.


Heshima ishi mda mrefu,
siikubali dhana potofu,
wadogo wajulia wapi machafu,
wenye umri wacheza rafu,
umri si mali kitu,
hekima yategemea utu.


Poleni kina dada,
wenye umri kuwawinda,
hekima gani kuwahadaa,
wanaukombozi twajiandaa,
njuga twalivalia,
unyanyasaji kijinsia,
hekima upeo tutajionea,
hekima umri tutashuhudia,
hekima utajiri tutatambua.


Angalizo tilieni maanani,
wako wakubwa wenye hekima jamani,
hekima zao zatufaa maishani,
dhana potofu nataka ondoa vichwani,
gumu lako jambo,
akuzidi'ye mwaka mwisho wa gumzo,
hekima, umri ni fimbo,
hekima, upeo ni nguzo.


Sijachoka kuandik…