Posts

Showing posts from March, 2009

TULIANGAZIE HILI

"kufaulu kwa mwanafunzi si kipaji bali utayari wake katika masomo"

Hivi kweli kwa masomo yote ayasomayo mwanafunzi hapatakuwepo na ambayo hataweza kuyamudu au tu ni kutokuwa tayari kusoma? Vijana wengi siku hizi wanaona kwenda shule ni utaratibu/sheria,ilimradi tu wamefika shule na wameonekana, kwa maana kwamba hawana malengo yoyote.Ni wachache sana wanaofahamu nini maana ya kwenda shule.Pengine wazazi/walezi pamoja na walimu wanawajibu wa kuwakumbumbusha wanafunzi wanatakiwa wafanye nini na ni yapi hasa malengo ya elimu iliyokusudiwa.

Wewe unaonaje?

Karibu sana.

Umeshajitambua/jielewa?

Kama ndio, umetumia vigezo gani?
Kama bado, kwa nini?
Ukweli ni kwamba wapo wanaoishi ktk maisha ya kujielewa/kujitambua lakini hawafahamu kuhusu dhana hii ya kujielewa, hawa wamejielewa? Mimi nafikiri hawajajielewa.

Pia wapo ambao hawayaishi maisha ya kujielewa na wala hawajui kuwa kuna kujitambua/kujielewa, hawa nao hawajielewi.
Mtu atajitambua vipi? Vigezo gani atumie kufahamu kuwa amejielewa?
Mimi nafikiri kujielewa hakuna mipaka bali ni kama kujifunza kusiko na mwisho. Tunatakiwa kila kukicha tuongeze kiwango chetu cha kujielewa.
Kujielewa ni namna ambayo humfanya mtu kuufikia ukamilifu(perfectness) ktk maamuzi, uhusiano na watu,utendaji kazi na uhusiano wa mhusika na mazingira kwa ujumla.

Namshukuru Bwaya kwa Falsafa yake hii ya jielewe kwani kupitia kwake nimeweza kujifunza mengi na ndio maana nimeweza kupata changamoto nyingine(zaweza kuwa ni ngeni au ni za kawaida) ambazo nazo zikijadiliwa zinaweza kuleta uelewa zaidi.

"kujitambua hakuna mwisho lakini jitahidi kuongeza kiwan…

Nimesikia mengi lakini hili! lanitisha.

Duniani inaonekana kuna mengi ni vile tu hatuwezi kuyafahamu yote.
Eti watoto waliozaliwa mapacha,mmoja akifa huwa hakuna matanga?
Kwani nilisikia siku moja watu wakiliongelea hili.
Katika maongezi yao niliwasikia wakisema kuwa siku ya matanga ni siku ambayo mtu aliyefariki husahauliwa kabisa na kuamini mtu yule hayuko tena duniani na ndio maana hata kila chake kinachoweza kurithiwa hugawanywa siku hiyo(sina hakika kama hii ni definition nzuri ya matanga,ni kwa mujibu wao).Mmoja wao aliendelea kusema kuwa kama matanga yatafanyika basi pacha aliyebaki atafariki tarehe na mwezi ambao pacha mwenzake alifariki lakini mwaka unaofuata.
Binafsi siliamini hili lakini niliachwa na mshangao mkubwa na maswali mengi;
je hii ni imani ya hawa wachache?
Kipi hasa kinachowaunganisha wawili hawa? na hali hii kuwakuta kama kuna ukweli?
Sayansi ina nafasi hapa?
Kwa bahati mbaya sikuweza kuhojiana nao kuhusu hili na nakaona ni bora niliweke hapa na kama kuna mwenye wazo lolote kuhusu hili atuwekee bayana.

Sikio ling'atwe wakati gani?

Kumnong'oneza mtu ni kumwambia jambo ambalo ni la usiri,ambalo linatakiwa kujulikana na watu wachache kwa kadiri iwezekanavyo.
Hivi kuna maana gani ya kumng'ata mtu sikio mbele za watu?
Likitokea jambo baya ktk yale mazingira,wanong'onezanao hadharani hawawezi kuwa matatani?

Wakisogea sehemu isiyo na watu, kuna haja tena ya kunong'onezana?


Mimi nadhani kumnong'oneza mtu ni mwanzo wa kufichuka kwa siri iliyotaka kufichwa.

Siku ya wanawake duniani; changamoto tatu.

1. Uwezeshwaji wa wanawake(women empowerment) dhana hii inawasaidiaje wanawake?
Sio kwamba dhana hii inaweza kuwapa kiburi ktk kujituma?
Wanawake kuikubali dhana hii si kwamba wamekubali kwamba wao ni wadhaifu?
Viongozi wanawake walipata uongozi kama kuwezeshwa,au kwa vile walionyesha uwezo ktk utendaji wa kazi?


2. Katika ndoa kuna dhana ya mwanaume kuchukuliwa kama kichwa na mwanamke kama mkia.Wawili wameungana na kuwa kitu kimoja,matabaka haya ya nini? Mwanamke kufananishwa na mkia kuna maanisha yeye atatakiwa kufuata ya mme wake.
Kwa wanaopendana kweli kuna umkia na ukichwa?
Kwa nini ukichwa na umkia?


3.Katika kuanzisha uhusiano wa kimapenzi inaonekana wanawake huwa wanasikiliza tu sera za wanaume,na kisha huzipitia na kukubaliana au kutokukubaliana nazo,yani sisi wanaume ni kama wanasiasa wanaonadi sera zao ili wakubalike kwa wapiga kura,hapa namaanisha kwamba wanawake hawana nguvu ya kumwambia mwanaume kuwa anampenda.Pengine labda ukichwa na umkia ndio unaanzia huku?
Au sababu wanaume nd…

Nikiwazacho.

"hekima haiko huru, inategemea sana na muktadha au mazingira"


"wisdom does not stand on its own, it largely depends on the situation"

tafakari kuhusu hili,niambie kuna ukweli kiasi gani, unaweza kulitumia wazo hili ktk maisha?

TAFAKARI YANGU

"mtu mwenye hekima ni yule mwenye uwezo wa kufikiri kwa haraka na kutoa jibu ambalo ni fasaha" kissima.

"a wise person is the one with fast thinking and with accurate solution" kissima.

Unaweza kukubaliana au kutokukubaliana na msemo huu, onyesha msemo huu una ukweli kwa kiasi gani, unaweza pia kupendekeza msemo wako mwenyewe(yasiwe mawazo ya mwingine) unaohusiana na hekima.
Amani,furaha na upendo vitawale kati yenu.