Posts

Showing posts from January, 2009

HALI HIZI ZINAPELEKANA PABAYA, ZISAIDIANE VIPI?

Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya wanafunzi wanasomea shida.
Hali hii hupelekea asilimia kubwa ya wanafunzi na wanajamii kuichukulia elimu kama njia ya pekee ktk kuondokana na umasikini.

Umasikini ni miongoni mwa sababu ya msingi sana inayopelekea mfumo duni wa elimu hapa Tanzania, wakati huohuo elimu duni hii tunayoipata ktk mfumo huu duni ndio hiyohiyo inayotegemewa ktk kuuondosha umasikini tulionao.

Hali mbaya ya uchumi wa nchi(lakini mabilioni ya EPA kupotea bila serikali kugundua! Kulipa kampuni hewa, richmond,mafisadi,nk, vyote hivi vinahusisha pesa za serikali, muda wote serikali isigundue ufujaji huu mkubwa wa pesa! kama kweli hali ya uchumi haijakaa vizuri?) unasababisha mashuleni kusiwepo na vifaa vya kutosha ktk kufundisha,maabara za kisasa zenye kila kitu muhimu,nyumba bora za walimu,maktaba zenye vitabu vya kutosha na vyenye kukidhi haja za wanafunzi,nk.
Cha kushangaza watanzania masikini.masikini ndio tunashurutishwa tena kujenga mashule wenyewe(shule za kata) na kuyaend…

HIVI AMANI INAYOONGELEWA NI IPI?

Tanzania inaaminika kuwa ni miongoni mwa nchi zenye amani na utulivu barani Afrika na hata ulimwenguni kote.
Na ndio maana hata viongozi wetu mbali na (pengine) vipaji walivyojaliwa na Mungu hupewa nafasi ya kuwa wasuluhishi katika nchi nyingine hususani za kiafrika.
Migogoro ya kielimu kuanzia shule za msingi hadi elimu ya juu,kwa msisitizo ,vurugu iliyopo sasa kati ya Vyuo vikuu na serikali,
Wastaafu wanavyohangaikia mafao yao miaka nenda rudi bila mafanikio,watu wenye ulemavu wa ngozi(albino) wanavyoishi kwa uhuru mdogo mara mia pungufu ya ule alionao swala awapo kwenye mbuga yenye simba wenye njaa,wananchi wanaokufa kwa njaa huku wakubwa wakiisahau njaa na kuneemeka kwa jasho la huyu huyu mnyonge,umasikini uliokithiri mpaka umekuwa kama utambulisho wetu kwa mataifa mengine,ufisadi uliokithiri ambao naweza kuufananisha na dactari anayepiga operesheni bila ganzi,yani hana huruma ya utu hata kidogo,
Haya ni maeneo machache nimeyagusa,mtanzania mwenzangu una mifano hai mingi sana! Sisi…

BAADA YA KICHAA KUPEWA RUNGU.

Leo katika pitapita zangu katika mji wa Moshi nilikutana na kisanga kimoja ambacho kilinifanya niwe na hisia za aina yake kuhusiana na hawa waliopewa jukumu la kuangalia ama kusimamia usalama wetu.

Kabla ya kushuhudia kisanga hicho, katika pitapita nilifanikiwa kuwaona makuruta(recruits) vijana wanaopata mafunzo ya upolisi katika chuo cha polisi(ccp)tawi la Moshi.Nafikiri vijana hawa wanakaribia kutunukiwa vyeti vyao vya upolisi na wako kwenye mafunzo kwa vitendo.

Nikiwa nimeweka pozi sehemu fulani,mara niliona kundi kubwa la wanausalama hawa watarajiwa takribani ishirini hivi wakiwa wanawakokota vijana wanne huku wakiwa wamefungwa na kuunganishwa pamoja kwa kutumia mashati yao(kimsururu,yani kwa kufuatana),huku mkong'oto wa hapa na pale ukiendelea,


Nilijiuliza,hata kama mtu kakosea ndio achukuliwe kinamna ile kweli,? Kwani pale waliuondoa utu wa mtu kabisa kabisa!!

Nikajiuliza tena,au ni namna ya kupunguza hasira za mazoezi makali wayapatayo chuoni? Kama vijana walikuwa wanaleta …