Posts

Showing posts from October, 2015

Elimu inayozingatia uwezo(Competence Based Education): Maana na Misingi yake Mikuu

Image
Matumizi ya TEHAMA ni moja ya njenzo muhimu ya kufanikisha Elimu inayozingatia uwezo mashuleni. Kupitia TEHAMA, wanafunzi wanaweza kujisomea popote na kwa wakati wao huku wakishirikiana na wenzao popote pale walipo. Picha kutoka HakiElimu Kama nilivyotangulia kuandika katika makala iliyotangualia, ni takribani miaka kumi na ushei tangu elimu inayozingatia uwezo ilipoanza kutumika rasmi nchini Tanzania. Katika kipindi hiki, hakujakuwa na mafanikio ya kuridhisha sana katika ngazi zote za elimu.  Wanafunzi wengi wanamaliza elimu ya msingi bila kujua kusoma wala kuandika, wanafunzi wengi wanamaliza shule za sekondari wakiwa wamepata madara yasiyoridhisha. Vile vile, vijana wa vyuo vikuu wanamaliza vyuo bila kuwa na stadi stahiki za kukabiliana na changamoto za kukosekana kwa ajira n.k. Elimu inayozingatia uwezo ilitazamiwa kuwa ingeweza kukabiliana vyema na changamoto hizi za kufeli kwa wanafunzi pamoja na suala la ajira hususani kwa vijana wanaomaliza vyuo vikuu. Laki

Elimu Inayozingatia Uwezo: Bado Inasuasua, Wapi tunakosea?

Image
Picha kwa hisani ya gettingsmart Elimu inayozingatia uwezo imeshika kasi zaidi kipindi cha hivi karibuni, hususani kwa mataifa ya Ulaya. Nchi kama Marekani imewekeza kiasi kikubwa cha fedha kuhakikisha elimu hii inatumiwa mashuleni na vyuoni ili kuleta ufanisi unaopaswa. Kwa mfano,   blogu ya BlackBoard kwa kushirikiana na Baraza la Elimu la Marekani , tayari wameungana kufanya Tafiti za Elimu Inayozingatia Uwezo . Utafiti wa hivi karibu wa BlackBoard na Baraza la Elimu la Marekani umejaribu kuangalia ni kwa kiasi gani Elimu Inayozingatia Uwezo inavyoweza kutekelezwa na pia mafuaa yake kijamii na kisera na namna ambavyo mfumo wa krediti na uwezo unavyotafsiriwa na wadau mbalimbali wa elimu. Kutokana na ukweli kwamba, kiwango cha elimu nchini Tanzania kwa kipindi kirefu kimekuwa kikidorora kadiri siku zilivyokuwa zinaenda, moja ya muarobaini ulionekana ni kuazima mfumo wa Elimu unaozingatia Uwezo.   Hivyo basi, mwaka 2004, Tanzania kupitia Taasisi ya Elimu iliamua kubadi

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?