Posts

Showing posts from September, 2014

Utaratibu Huu wa Kuoa/Olewa ni Mzuri, Unahitaji Kuboreshwa Kidogo.

Image
Picha kwa hisani ya Gospel Kitaa. Hakuna asiyejua shughuli ya kuoa/olewa ilivyo na pilika pilika nyingi na za kuchosha.   Siyo tu hupoteza muda na fedha, mara nyingine huishia kwa watu kugombana, kuwekeana chuki na vinyongo visivyoisha.   Asilimia kubwa ya fedha za harusi hutokana na michango ya watu mbalimbali kuanzia ndugu, jamaa na marafiki. Harusi ni sherehe ifanywayo kwa ajili ya kufurahia tukio muhimu la kufunga ndoa. Sherehe hii huja mara baada ya wapendanao   kufunga ndoa   kanisani, msikitini, serikalini ama kwa utamaduni.   Hadi siku ya ndoa, sherehe ndogo ndogo za awali kama za kutambulishana, yaani ndugu wa pande mbili kufahamiana, kuvishana pete za uchumba, utoaji wa mahari, kapu la mama na send off   hufanyika. Sherehe ya awali kabisa inayowashirikisha watu nje ya familia ni kapu la mama. Sherehe hii ni sehemu ya maandalizi ya sherehe ya kumuaga msichana (mara nyingi hufanywa upande wa msichana). Hapa mama wa msichana ndiye mhangaikaji mkuu. Hugharamia kiasi

Moja ya Matatizo Yanayoikumba Sekta ya Elimu ni Kukosekana kwa Uwajibikaji.

Image
       Vyoo vya kutegemewa katika moja ya shule za sekondari hapa Tanzania Madhara ya kukosekana kwa uwajibikaji Uwajibikaji ni moja ya dalili kuu ya Uzalendo. Mtu aliye na sifa ya uzalendo, lazima awe muwajibikaji. Sekta nyingi hapa Tanzania zinashindwa kupiga maendeleo yenye tija kwa sababu mbalimbali, mojawapo na iliyo kuu ni kukosekana kwa uwajibikaji. Lengo la makala hii, ni kujadili viashiria kadhaa vya kukosekana kwa uwajibikaji na uwajibishwaji katika sekta ya elimu nchini Tanzania. Wadau wote wa elimu kuanzia serikali na mamlaka zake husika, wakuu wa shule, walimu, wazazi/walezi, jamii na wanafunzi wenyewe wnahusika katika suala la uwajibikaji. Kila kundi lina nafasi yake na wajibu wake katika kufikia malengo yaliyokusudiwa. Muhusika wa kwanza anayepaswa kuwajibika ni mwanafunzi mwenyewe. Kuna ule msemo usemao, “unaweza kumlazimisha punda kwenda mtoni, lakini siyo kunywa maji”. Shule inaweza kuwa na mazingira rafiki ya kusomea, walimu wa kutosha na walio na

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Image
Umbali kati ya shule na waishipo wanafunzi, hususani kwa shule za kutwa, umebainishwa na watafiti wa elimu kuwa unaathiri masomo ya mwanafunzi. Picha kutoka Fullshangwe Blog . Imetumiwa bila ruhusa. Kama nilivyodokeza katika makala iliyotangulia, makala hii inajadili mambo kadhaa ya msingi ya kuzingatia ili kuboresha na kuongeza ufanisi wa shule, hususani za msingi na sekondari. Mambo haya ni matokeo ya tafiti mbalimbali za masuala ya uboreshaji na ufanisi wa shule. Ubora wa elimu Tanzania umeendelea kushuka siku hadi siku, na mikakati kadhaa ikiwamo ya matokeo makubwa sasa imeanzishwa katika kukabiliana na changamoto hii.. Harakati yoyote ya kuboresha ufanisi na ubora wa shule hauna budi kuzingatia mambo kadhaa yakiwemo haya takayoyajadili hivi punde kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kielimu. Uongozi bora Tafiti za masuala ya ufanisi wa shule zinaonesha kuwa, wakuu wa shule wamekuwa kiini cha mafanikio ya shule.   Tafiti hizi zinaonesha kuwa, ubora wao hufikiwa pale wana

Tunawezaje Kuongeza Ufanisi na Ubora wa shule? Watafiti wa Masuala ya Ubora na Ufanisi wa Shule Wanatujuza.

Image
Wanafunzi wakiwa wamekaa chini darasani huku somo likiendelea katika moja ya shule za msingi mkoani singida.  Kwa kipindi kirefu sasa, shule za msingi na za sekondari za Tanzania zimekuwa na matokeo yasiyoridhisha.   Kuna idadi kubwa ya watoto wanaomaliza elimu ya msingi pasi kujua kusoma na kuandika. Hali kadhalika, wapo vijana wengi wa sekondari wanaomaliza na kushindwa kupata alama stahiki za kuwawezesha kuendelea na elimu ya juu. Kufuatia hali hii, yapo mengi   yaliyozungumzwa na mikakati kadhaa kufanyika. Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kuweka utaratibu wa kuandaa walimu wengi wa elimu ya awali kwa shule za msingi. Katika kukabiliana na changamoto za uhaba wa walimu hasa wa sayansi kwa shule za sekondari, mikakati kama ya kutumia teknologia katika ufundishaji na ujifunzaji imeanzishwa.   Wanafunzi wa shule moja ya msingi mkoani singida wakisomea katika darasa lisilo na ubora kabisa. Kuhusu ubora wa shule, kuna mambo mengi yamefanyika. Kwan

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?