Posts

Showing posts from March, 2012

Shule za Msingi za Vijijini- hali bado ni tete!

Image
Ni wiki moja sasa imepita tangu nilipomaliza zoezi la kukagua maendeleo ya waalimu tarajali wanaoendelea na mafunzo yao ya kufundisha ya muda mrefu yaani "block Teaching Practice" (B.T.P). kazi ilikuwa ngumu kwani iliambatana na changamoto nyingi. shule nyingi zipo vijijini na miundo mbinu ya barabara bado ni tatizo kwa sehemu nyingi za wilaya ya Iramba. Pamoja na changamoto nyingi nilizokabiliana nazo wakati wa zoezi hili, nimepata fursa ya kutembelea maeneo mengi ya vijiji vya wilaya ya Iramba na wilaya ya Singida Mjini kwa uchache. Nimepanua jiografia na kujifunza mambo mengi . Leo nitaeleza japo kwa ufupi, hali ya shule zetu za Msingi. Mazingira ya shule za msingi za Iramba bado hayaridhishi. Bado kuna idadi kubwa ya watoto wanaokaa chini. Kwa bahati mbaya madarasa ambayo wanafunzi wanakaa chini, hayana sakafu. Mfano, katika Shule ya Asanja iliyo wilaya ya Iramba, kuna madarasa ambayo hayajaezekwa, wanafunzi wanakaa chini. Pia kuna shule moja katika manispaa ya Singida,

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?