Posts

Showing posts from July, 2011

Hii ni Sayansi au Imani?

Image
Kuna mambo mengine katika hali ya kawaida, tunayatenda lakini kuyaelezea inakuwa vigumu. Tunatumia dawa na kusubiri kupona. Wengine wanatumia chakula na kusubiri wapate nguvu na kuona miili inajengeka. Maelezo ya nini kinatokea hadi haya yanafanyika, mara nyingi yanakuwa si muhimu. Picha hapo juu, inaonesha gunzi likiwa limefungwa kwenye shina na mpapai. Madhumuni ya gunzi hili ni kuzuia mpapai usiwe dume kwa maana ya kutoa maua ambayo yatatoa mapapai yasiyo ya kawaida na ambayo hayatafaa kuliwa.Nami nilishawahi kutumia njia hii miaka fulani iliyopita. Ni kweli mipapai ilikuwa inabadilika; kutoka mipapai dume na kuwa mipapai yenye kutoa mapapai mazuri yenye kufaa kula. Mapapai dume huwa yanakuwa marefu isivyo kawaida na huwa hayafai kula. Ninachojiuliza hapa ni kuwa, gunzi hili linafanyaje kazi? Labda hii ni Sayansi na pengine yapo maelezo ya kinachotokea. Au labda, hii ni imani. Kwa maana kuwa gunzi halina msaada wowote, kwamba kingine chochote kingeweza kufungwa na muhusika ak

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?