Kadiri siku zinavyoenda, nazidi kujionea namna ambavyo serikali yangu ya Tanzania inavyoonesha udhaifu mkubwa katika masuala mengi ya utendaji wake. Katika pita pita zangu, nilikutana na jengo moja lililopo katika kijiji cha Kyalosangi kilichopo wilaya ya Iramba katika tarafa ya Kinampanda mkoani Singida. Nililisogelea karibu na kisha nilikiona kibao kama kinavyoonekana hapa chini katika picha ambacho kilinitambulisha kuwa ni mahakama ya mwanzo. Nilistaajabu maana jengo hili linaonenaka kama ni gofu na ni mda mrefu sana umepita bila kutumika. Nilfanikiwa kuomgea na mkazi mmoja na alinieleza kuwa mahakama hii inatumika na kwa bahati nzuri nami siku moja nilishuhudia watu wakipata huduma mbalimbali katika mahakama hii iliyo katika hali ya kusikitisha kwa namna jengo hili lilivyochakaa kana kwamba haina uangalizi wa aina yoyote wa wananchi na serikali .
Hiki ni kibao kinachoelekeza mahali ilipo Mahakama ya Mwanzo, Kinampanda wilayani Iramba katika Mkoa wa Singida.
Picha hapa juu ni mwonekano wa Mahakama hii. Bado inatumika kwa shughuli za kimahakama pamoja na kuwa inanonekana kama jengo lililotelekezwa miaka mingi iliyopita.
Picha hapa chini zaonesha sehemu ya ndani ya mahakama hii.
Sehemu ya kukaa watu katika harakati za kupata huduma mbalimbali mahakamani hapo
Ni dhahiri kuwa watendaji na wasimamizi wa mahakama ni wazembe. Hili halina mjadala. Ni aibu kubwa kwa Serikali yangu ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni aibu kwa mahakama kuonekana kama Gofu na ilihali babo inatumika.
Pengine labda serikali inasubiri jengo hili lianguke kabisa na pengine kusababisha hata maafa (kwani siku moja laweza kuwaangukia watu wakiwa mahakamani) kisha waseme imeshatokea na hakuna namna nyingine zaidi ya kufidia wahanga (kauli kama hizi zimeshazoeleka sana na tumezishuhudia kwenye matukio mengi yakiwemo ya milipuko ya mabomu Mbagala na Gongo la mboto) na kuanza mchakato wa kujenga jengo jingine (au kutojengwa kabisa)la mahakama kwa gharama kubwa ambazo zingeepukika kwa kukarabati jengo lililokuwepo kwa kiwango kizuri na kwa gharama nafuu.
Fedha za walipakodi badala ya kuelekezwa kwenye majukumu kama haya ya kuboresha huduma za jamii, inaelekezwa sehemu nyingine ambazo hazina umuhimu kwa wakati huo (wabunge kupewa pesa kwa ajili ya kununulia magari yao binafsi ni mfano ulio hai).
Watumia mahakama hii (wananchi), labda kwa kutokujua ama akili zao kufungwa na mazoea, hili hawajaliona kama ni tatizo. Labda bado wapo kwenye ule utaratibu wa bora maisha kuliko maisha bora, au wale wa kushukuru siku imepita na bila hata kutathimini imepitaje, ama wale wa bora nimekula hata kama ni ugali wa chumvi. Jamii ya mawazo haya bado ipo miongoni mwetu na haina budi kupitwa na watati.
Huu ni uteandaji mbovu kabisa wa serikali yetu ya Tanzania, yaonesha kiwango kisichoridhisha kabisa cha utendaji. serikali isisubiri wananchi wawe wazalendo maana yanayotokea Misri na kwingineko hayataepukika. Wananchi nasi hatuna budi kufungua midomo yetu, hatuna budi kuonesha kutoridhika na huduma duni katika sehemu husika.

4 comments:
Kwa kweli inasikitisha sana.
Sasa hapo ndipo nyumba ya kutafutia haki...labda ndio sababu ipo hivyo, kwani haihitaji `umaridadi ' kwani wanaoletwa hapo ndio akina sisi, hata ndala kununua shida!
inasikitisha sana hata mtuhumiwa anapata hofu ya kushitakiwa kabla hata kesi haijasomwa,sababu mazingira yamekaa kiufisadi inaonyehsa kunakarushwahapo.
Hali hii haitofautiani kabisa na ile ya shule nyingi za msingi hapa Singida. Nimezitembelea shule kadhaa, hali inatisha, ni mazingira yakatishayo tamaa, si kwa wanafunzi, hata kwa waalimu wa shule hizo.
Post a Comment