Ulimwengu wa kublogu unazidi kushika kasi hasa hasa katika kipindi hiki ambacho huduma ya intaneti inavyozidi kupatikana kwa urahisi. Ni jambo la kujivunia kuwa kila siku watu wanazidi kujumuika katika kuielimisha jamii kwa njia ya mtandao na hususani kwa njia hii ya magazeti huru ya mtandaoni, na kila mmoja kwa namna yake aonavyo inafaa.
Basi, leo hii naomba kumtambulisha ndugu David Mgaya ambaye naye kwa kupitia mashairi, ameona analo jambo la kutuelimisha wanajamii. Ndio kwanza anaanza, lakini ni imani yetu kuwa anayo mengi ya kutufunza na kutuburudisha. Waweza kubofya hapa ili upate kuona kile akusudiacho kujifunza nasi.
Karibu sana ndugu Mgaya.

3 comments:
Kaka Albert ahsante sana kwa kutujuza ngoja niende huku kumsalimia..David Karibu sana katika ulimwengu huu wa kublog:-)
Tumeshamkaribisha. Asante kwa kumtambulisha.
Karibu Mshairi!
Post a Comment