...binafsi hauniumizi kichwa, kwani lengo langu ni kuona chama tawala na wanaokijenga wanabwaga manyanga.
.....natamani kuona chama cha upinzani kikishika hatamu. Natamani kuona upande wa pili wa shilingi.
.....sina haja ya kusikiliza chama tawala kinasema nini kwenye kampeni zake kwani wameongea kwa miaka mingi na bado hali ya taifa letu hairidhishi.
.....nashangaa kuuona umati mkubwa wanaoshangilia kwenye kampeni za chama tawala. Hawa hawa ndio wale wanaolalamika kuhusu hali duni ya maisha inayowakabili pamoja na kuwepo kwa neema kubwa ya hazina ya rasilimali nyingi ndani ya nchi yetu.
......nawaza kama maendeleo ya taifa letu yanayojongea kwa mwendo wa kinyonga unawiana na miaka yooooote ya utawala wa chama tawala baada ya uhuru hadi leo hii.
......nawaza kama watanzania tunajua tulipotoka, tulipo na tunapokwenda ili tupate kujua kuwa tunahitaji mabadiliko ya utawala na watawala wa chama tawala au la.
.....Natamani kumwona Dr Slaa anachukua kiti cha uraisi. Huu ndio upande mwingine wa shilingi ninaoutamani. Sukari haionjwi kwa kuitazama, wala chumvi, wala pili pili. Natamani kuona upitanzani utafanya nini. Asemayo Dr Slaa si kigezo kwangu, natamani kuona atafanya nini. Natamani watu wangeniunga mkono kwa wazo langu hili. Natamani watu wangelitamani badiliko hili bila kujali sana kile Dr Slaa akisemacho kwenye kampeni zake japokuwa ayasemayo ni muhimu katika maamuzi ya mpiga kura. Chama tawala si kimeshasema mengi? Mimi nadhani yanatosha sana.
Uchaguzi wa mwaka huu.....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

9 comments:
umeongea mengi mazuri lakini hili limenigusa nasa nalinukuu "Natamani kumwona Dr Slaa anachukua kiti cha uraisi"
chadema wakipata kura moja basi mjue ni ya kwangu
Nashukuru Anony, pamoja sana. Mabadiliko yapo mikononi mwetu na uamuzi ni wetu sisi watanzania.
Bwana Albert tuombe Mungu afanikishe mageuzi yatakayotuletea maisha bora baada ya uchaguzi.
Ni kweli ndugu Msengi. Maisha bora yapo mikononi mwetu. Kwa Tanzania yetu, maisha bora kwa kuendelea na asilimia kubwa ya wanaCCM bado naona ni ndoto. Namaanisha, chama si tatizo, tatizo ni viongozi ndani ya chama. Dr Slaa angekuwa mwanaCCM ni dhahiri asingeweza kufanya aliyokwisha yafanya. Wazalendo wanaikimbia CCM kwani haijali maslahi ya nchi bali maslahi binafsi. Ni vile tu wananchi wengi hawajui mwenendo wa chama tawala, wapo kishabiki tu.
duhu mabadiliko ni lazima tu
@kaka Kamala, kama sisi wapiga kura ndio tumeamua hivyo, basi mabadiliko hayatakwepeka.
Safi sana mzee lakini tunapendelea habari hizi zingekua na picha za SGD.
Mhh, natamani kila Mtanzania siku hiyo angefika kupiga kura yake ili mwisho wa siku kila mmoja abebe dhamana yake.
Anony, taratibu tuu, soon and very soon.
Ni kweli emu-three, kura yetu ni muhimu, hata na umoja wetu pia. Huwa ninawaza kama ni kweli Odinga alishinda au hakushinda, na kama alishinda, wananchi walijuaje na waliweza vp kuungana na kumkutetea? au ni wananchi walirubuniwa ktk kumtetea Odinga ili angalao apate uwaziri mkuu? Duh! Umoja wa wapiga kura nao ni muhimu.
Post a Comment